Sunday, 22 March 2015

Kitabu; Kwa Nini Mpaka Sasa Wewe Sio Tajiri.

Waswahili wanasema huwezi kutatua tatizo usilolijua. Baada ya kufuatilia kwa kina sana kuhusiana na jitihada za watu kuondoka kwenye umasikini na kuwa matajiri nimegundua kwamba wengi wetu tunajaribu kutatua tatizo tusilolijua.
  Unapojaribu kutatua tatizo usilolijua huishii tu kushindwa kutatua tatizo hilo bali unazidi kuwa kwenye hali mbaya zaidi kwa kukosa suluhisho na kuendelea kutafuta suluhisho huku ukizidi kupotea.
  Katika tatizo letu la umasikini tumekuwa tukijipa sababu nyingi sana kwa nini hatujaweza kuwa matajiri. Lakini asilimia tisini ya sababu hizo ni za uongo. Na hata hiyo asilimia kumi ambazo ni za ukweli bado hatuna suluhisho la sababu hizo.
kitabu kava
  Tunakuwa na sababu za uongo kwa sababu hakuna sehemu yoyote kwenye mfumo wa elimu tunakofundishwa jinsi ya kutengeneza utajiri. Na kwenye jamii kwa kuwa masikini ni wengi zaidi ya matajiri hakuna kikubwa tunachoweza kujifunza kutoka kwenye jamii.
  Kwa kukosa elimu hii muhimu watu tumekuwa tukienda kwa kubahatisha na kufanya majaribio mbalimbali ya kutufikisha kwenye utajiri. Kwa kutokuwa na elimu ya kutosha mengi ya majaribio tunayofanya yanazidi kutupoteza na kufanya maisha yetu kuwa magumu zaidi.
  Kwa kuona umuhimu wa elimu hii kwangu na kwa watanzania wenzangu nimeandika kitabu kinachoitwa KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIO TAJIRI, sababu ishirini na tano zinazokuzuia wewe kufikia utajiri. Kitabu hiki kipo kwenye mfumo wa softcopy wa PDF na unaweza kukisoma kwenye kompyuta yako au simu yako kama ina uwezo wa kusoma vitabu.
kitabu kava2kitabu kava3
Kitabu hiki ni kifupi sana, kina kurasa 81, ila kimejaa mafunzo ambayo kama ukianza kuyatumia utaona mabadiliko makubwa sana kwenye maisha yako. Nimejitahidi kukifanya kitabu hiki kuwa kifupi ili hata wale ambao ni wavivu wa kusoma waweze kusoma kitabu hiki. Pamoja na kuwa kifupi, mafunzo yaliyopo ndani yake ni makubwa sana na unayahitaji sana ili uweze kutoka hapo ulipo.
  Kwenye kitabu hiki utajifunza sababu ishirini na tano kwa nini mapaka sasa wewe sio tajiri. Na pia kwenye kila sababu utajifunza ufanye nini ili uweze kuondoka kwenye umasikini na kuingia kwenye utajiri.
  Kitabu hiki kitapatikana kwa gharama ndogo sana ya shilingi za kitanzania elfu tano(5,000/=) ili kila mtanzania aweze kukisoma na kutumia mafundisho hayo kuboresha maisha yake.
  Kupata kitabu hiki tuma fedha tsh elfu tano kwa tigo pesa(0717396253) au mpesa(0755953887) na kisha tuma email yako kwenye moja ya hizo namba na utatumiwa kitabu chako. Kwa mawasiliano zaidi unaweza kutumia namba hizo au email amakirita@gmail.com
  Wahi upate kitabu hiki mapema ili uendeleze mabadiliko makubwa kwenye maisha yako.
  Nakutakia kila la kheri na tuko pamoja kwenye safari hii.

No comments:

Post a Comment